Mamlaka ya mawasiliano Uganda yaamuru mitandao ya kijamii kufungwa.

Mamlaka ya mawasiliano ya Uganda imeyaamuru makampuni ya huduma za intaneti, kuifunga mitandao ya kijamii siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika. Katika barua ambayo shirika la habari la AFP limeipata, mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano ya Uganda UCC Bi. Irene Sewankambo ameyaagiza makampuni ya mawasiliano kusitisha mara moja matumizi ya mitandao ya kijamii na